| MADAI YA MGOMO WA WANAWAKE WA DUNIA. -Malipo kwa kazi zote za kutunza-katika mshahara, kiinua mgongo,ardhi na raslimali nyingine. Kuna nini chenye thamani zaidi ya kulea watoto na kuwatunza wengine? Tuwekeze katika maisha na ustawi wa jamii; sio katika bajeti za majeshi au wafungwa. -Malipo sawa kwa wote, wanaume na wanawake katika soko la dunia. -Malipo kwa likizo ya uzazi, mapumziko ya kunyonyesha na maslahi mengine-acheni kutuadhibu kwa kuwa wanawake. -Kukomeshwa kwa "Madeni ya Nchi za Dunia ya Tatu" ambayo yamewaangukia sana wanawake na wasichana. Tunadai zaidi ya "tunavyodaiwa." -Upatikanaji wa maji safi, huduma za afya, nyumba, usafiri na elimu. Nishati isiyochafua mazingira na teknolojia inayopunguza saa za kazi. Sote tunahitaji majiko, mafriji, mashine za kufulia nguo, makompyuta na muda wa kupumzika! -Ulinzi na hifadhi kutokana na vipigo na mateso ya aina yoyote ikiwa ni pamoja na yale ya wanafamilia na watu wenye nafasi za madaraka. -Uhuru wa matembezi. Kusafiri huru ....kwa nini bwana?!? |
Mgomo wa Wanawake Doniani (leaflet)
Ukurasa wa nyumbani (homepage)
Wasiliana nasi (contact us) Kampeni ya Kimataifa ya Mishahara kwa kazi za Nyumbani. Kituo Cha Wanawake Njiapanda