Mshahara wenye Kukidhi Mahitaji kwa wakina Mama na Walezi wote

Wapendwa Mabibi na Mabwana,

Tuwajali wakina mama, Tuwajali Walezi wote

Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu, tunazindua Maombi maalum ya Kimataifa ya kudai mishahara ambayo itawawezesha wakina mama wote na walezi wote duniani kuweza kukidhi mahitaji yao ya kila siku (tazama chini).

Kulea ni msingi wa kila jamii; hata hivyo kazi hii, ambayo hufanywa zaidi na wanawake, haithaminiwi, ina malipo kidogo au wakati mwingine haina malipo kabisa.

Wanawake wanafanya karibu theluthi mbili (2/3) ya kazi zote duniani. Baadhi ya wanawake wameweza kuendelea na kuwa wataalam katika nyanja mbali mbali kama wanasiasa na wengine hata wameweza kujiunga kwenye asilimia moja (1%) ya dunia ambayo ni tajiri zaidi na inaendelea kuwa tajiri. Lakini wanawake wengi, hasa wakina mama, bado inawawia vigumu kuweza kujikimu wao na wapendwa wao.

Kuwekeza na kuwalipa vizuri wale wanaofanya kazi za uleaji, itasaidia kupunguza pengo la kipato kati ya wanawake na wanaume.

Pia, itasaidia kuwavuta wanaume wengi katika kutoa huduma za malezi. Na zaidi sana, itasaidia kuelekeza sera za kiuchumi na kijamii kuelekea maisha bora, afya na ustawi wa jamii.

Wafanyakazi wote wana haki ya mshahara ambao utawawezesha kukidhi mahitaji yao ya kila siku. Kama sehemu ya juma la Kimataifa la Wanawake nchini Uingereza, tarehe 14 Machi, Tutawaenzi wakina mama, tutawaenzi walezi na watoa huduma zote za malezi - wanafanya kazi kwa bidii sana, ingawaje hawathaminiwi kabisa!

Tunatarajia kikundi chako kitaidhinisha ombi hili la kimataifa na kulisambaza kila mahali kwa ajili ya kutiwa saini. Ombi hili litarushwa hewani kwanye mtandao tarehe 14 Machi katika lugha mbalimbali – tunakaribisha tafsiri za lugha mbali mbali za ombi hili. Ila kabla ya kufanya hivyo tafadhali tutumie barua pepe kwanza.

Sisi pia tuna shauku ya kutaka kujua wakina mama wa walezi wengine wanaendeleaje katika nchi yako -changamoto zenu, magumu mnayopitia, ukandamizaji mnaokabiliana nao, na mafanikio yenu.

Tunataka kufanya kazi kwa pamoja ili kuinua hali za watu wote wanaofanya kazi za malezi duniani kote. Jamii ya binadamu, dunia na viumbe vyote vyenye uhai, haviwezi kuishi bila kulelewa na kuangaliwa na walezi.

Wekeza katika malezi, Wekeza katika mishahara yenye kukidhi mahitaji.
Selma James na Nina Lopez

 

Ombi kwa Serikali Zote

Mshahara wenye Kukidhi Mahitaji kwa wakina Mama na Walezi wote

Kulea ni msingi wa kila jamii. Hata hivyo, kazi hii ya kulea ambayo hufanywa zaidi na wanawake ina malipo kidogo au haina malipo kabisa na haithaminiwi ya kutosha.

Matakwa yetu ni kama ifuatavyo:

1. Kila mfanyakazi alipwe mshahara ambao utamuwezesha kukidhi mahitaji yake ya kila siku, ikiwa ni pamoja na wakina mama na walezi wote kwa ujumla.

2. Bajeti za kitaifa na za kimataifa zielekeze misaada ya kifedha na rasilimali nyingine kwa wakina mama na walezi wote kwa ujumla.

Sign here

Tunashinikiza mishahara ya kukidhi mahitaji ya kila siku kwa wakina mama na walezi kwa sababu zifuatazo:

• Kila mfanyakazi ana haki ya mshahara ambao utamuwezesha kukidhi mahitaji yake ya msingi ya kila siku. Wanawake kufanya theluthi mbili (2/3 )ya kazi zote duniani -ikiwemo majumbani, mashambani, na katika jamii kwa ujumla - lakini nyingi ya kazi hizi hazilipi vizuri.

Wanawake ni walezi wa msingi duniani kote, wakipigania kuhakikisha watoto, wagonjwa, walemavu na wazee, wanaishi vizuri na kunawiri. Wanafanya yote haya si tu kwenye yumba zao, bali hata nje ya nyumba zao, katika amani na katika vita . Wanawake wanazalisha sehemu kubwa ya chakula duniani.

• Walezi wengi, kuanzia wakina mama, hawapati mishahara kabisa na hawachukuliwi kama wafanyakazi.

Walezi wengi wenyewe ni walemavu, wengi wao ni watoto wanaolea watoto wenzao wadogo, au mama zao ambao hawajiwezi. Wengi wao pia ni wazee ambao wanaacha kustaafu ili wawezi kuwalea watoto wa watoto wao.

• Kulea ni kazi ngumu, lakini ujuzi unaohitajika hauthaminiwi katika soko la ajira. Kazi za ndani, huduma kwa wasiojiweza, kulea watoto na hata uuguzi hulipwa kima cha chini kabisa.

Tukianza kuthamini kazi za uleaji itasaidia kupunguza pengo la kipato kati ya wanawake na wanaume, na pia itasaidia kuwaleta wanaume wengi zaidi katika kazi za malezi.

• Kwa sababu walezi huwa hawalipwi mishahara, hii inapelekea wanawake wengi kunaswa katika mahusiano yenye vurugu kwa sababu hawana njia ya kuweza kujimudu kifedha.

Wakina mama wengi hufanya kazi zaidi ya moja na hapo hapo inawalazimu waweze kutafuta muda wa kuwa na watoto wao, hii inaleta usumbufu kwa kina mama na watoto.

• Wakina mama wanapokuwa maskini na wanapochoshwa na kazi, watoto huteseka na njaa, magonjwa, unyanyaswaji na unyonyaji.

• Wamama ambao inawalazimu kurudi kazini mara baada ya kujifungua, inawawia vigumu kuweza kunyonyesha watoto wao.

• Wafanyakazi ambao huchukua likizo ili waweze kuwahudumia watoto wao na wapendwa wao, hupoteza malipo, nafasi ya kupandishwa cheo, bima na pensheni.

• Kutoipa kazi za uleaji thamani yake halisi, inamaanisha hatuwathamini watu, mahususiano na maisha kwa ujumla.

• Kuwekeza katika walezi itasaidia kuelekeza sera za kiuchumi na kijamii katika maisha bora, afya na ustawi wa jamii - kwa ajili ya kila mtu na kwa ajili ya dunia ambayo inatumiwa na sisi sote.

JINA (ANDIKA & TIA SAINI): …..……………………………………………….…………...

SHIRIKA (KAMA LINAHUSIKA): …………………………………………………….………..

BARUA PEPE / NAMBARI YA SIMU: ………………………….………............................

JIJI & NCHI (SIO LAZIMA): …………………………………….……………….….............

ULIZA SHIRIKA / KIKUNDI CHAKO KUIDHINISHA: .....................................................

Imetolewa na: Global Women’s Strike (GWS) ● Women of Colour in GWS gws@globalwomenstrike.net www.globalwomenstrike.net 020 7482 2496
Crossroads Women’s Centre, 25 Wolsey Mews, NW5 2DX